UBORA WA MAKOCHA WA KLABU NI FAIDA KWA TIMU ZA TAIFA

MOJA ya sababu kubwa inayopelekea nchi yoyote kufanikiwa kisoka ni kuwa na timu bora au kama sio timu bora basi ni wachezaji bora.

Na kuna nchi nyingine huwa na timu bora na wachezaji bora kwa wakati mmoja. Mfano; kuna wakati Hispania ilibarikiwa kuwa na timu na wachezaji bora.

Mfumo wao wa tiki taka uliwataka wacheze kitimu na kuunda timu bora zaidi duniani. Lakini wakati huo huo, walikuwa na wachezaji bora uwanjani ambao akikosekana mmoja basi kuna nguvu inapungua katika eneo lake.

Nilibahatika kuushuhudia ubora uliotukuka kwenye miguu ya Xavi Hernandez ambaye bila shaka ndiye kiungo bora zaidi katika kizazi chake. Huyu mwanamume alikuwa ni roho ya Hispania, halafu na Barcelona. Hizo ni timu mbili kubwa nilizozishuhudia kwa mboni zangu mbili. Namshukuru Mungu kwa hilo.

Roho ya binadamu inapokata ghafla kila mtu anajua ni kipi kinachofuatia. Ndivyo sisi wanasoka tulivyokuwa tukigundua ni namna gani Barca au Hispania zitakavyokwenda kucheza bila uwepo wa Xavi.

Roho ya binadamu inapokata ghafla kila mtu anajua ni kipi kinachofuatia. Ndivyo sisi wanasoka tulivyokuwa tukigundua ni namna gani Barca au Hispania zitakavyokwenda kucheza bila uwepo wa Xavi.

Hata hivyo, timu hizo zingeweza kutafuta njia mbadala za kushinda mechi zao. Ndio maana ya timu bora inapopatikana.

Timu kama timu, haiwezi kujiendesha yenyewe bila kiongozi. Nyuma yao kuna kocha na jopo lake zima la ufundi. Huyu ndiye kiunganishi cha wachezaji hao wote kutoka klabu tofauti tofauti.

Halafu nyuma ya kocha wa timu ya taifa, kuna makocha mbalimbali wa hizo klabu. Hao sasa ndio chachu kuu ya mafanikio ya timu za taifa. Nitakupa mifano michache itakayotusaidia sote kuelewana hapa.

Halafu nyuma ya kocha wa timu ya taifa, kuna makocha mbalimbali wa hizo klabu. Hao sasa ndio chachu kuu ya mafanikio ya timu za taifa. Nitakupa mifano michache itakayotusaidia sote kuelewana hapa.

Brazil hivi sasa ipo chini ya kocha Tite, huyu jamaa ninaweza kusema na yeye ana mchango wake mkubwa tu wa kuwainua tena wachezaji walioonekana kupotea kama vile Marcelo na Paulinho.

Lakini Tite anapaswa kuwashukuru Pep Guardiola na Zinedine Zidane, kwa wachezaji wawili, Gabriel Jesus na Casemiro.

Jesus tunaweza kusema kama vile alikuwa mkali hata kabla ya kukutana na Guardiola, lakini kocha huyo amekikuza kiwango chake na kufikia levo ya kimataifa.

Jesus tunaweza kusema kama vile alikuwa mkali hata kabla ya kukutana na Guardiola, lakini kocha huyo amekikuza kiwango chake na kufikia levo ya kimataifa.

Tite anapaswa kumshukuru Zizzou kwa kumpa uhuru Casemiro wa kulimiliki dimba pale Santiago Bernabeu. Caseiro wa Rafa Benitez alikuwa rizevu tu, lakini Zidane alipokamata usukani, Mbrazil akalichukua dimba la chini na kufanya makubwa, hivi sasa amekuwa ni roho ya Brazil kwenye kiungo cha kukaba.

Taifa jingine ninaloona kocha wake anafaidika kwa wachezaji wake kunolewa na makocha bora wa klabu ni Ubelgiji inayofundishwa na Roberto Martinez kocha wa zamani wa Wigan na Everton.

Taifa jingine ninaloona kocha wake anafaidika kwa wachezaji wake kunolewa na makocha bora wa klabu ni Ubelgiji inayofundishwa na Roberto Martinez kocha wa zamani wa Wigan na Everton.

Ubelgiji ni moja ya nchi zinazotajwa kubarikiwa idadi kubwa ya wachezaji wenye vipaji wanaosakata soka kwenye klabu mbalimbali duniani.

Jan Vertonghen, Toby Alderweireld, Kevin De Bruyne, Eden Hazard, Mousa Dembele, Dries Mertens na Romelu Lukaku ni baadhi tu.

Wachezaji niliowataja hapo wote wanacheza kwenye klabu zenye makocha wenye uwezo wa hali ya juu. Toby na Vertonghen wako Spurs ya Mauricio Pochettino. De Bruyne ndiye yupo kwa Guardiola. Makocha wawili ambao sioni haja ya kuwaelezea sana kwa kila mtu anawafahamu.

Changamoto iliyokuwa ikiwasumbua sana Ubelgiji ni kushindwa kuwafunga vigogo. Ubelgiji inaweza kumpiga Andorra bao 5-0 lakini ikashindwa kufurukuta mbele ya nchi kama Ureno au Ufaransa.

Wana wachezaji (hasa washambuliaji) ambao kimsingi wanatakiwa kusimamiwa na ‘si makocha’ bali makocha bora.

Shukrani kwa mshambuliaji kama vile Mertens yeye kwa sasa anaichezea Napoli, klabu inayofundishwa na Maurizio Sarri ambaye wanamtaja kama kocha aliyeifanyia mapinduzi klabu hiyo na kuifanya iwe hatari Italia na bara zima la Ulaya.

Tunaweza kulalamika kwanini Taifa Stars haifiki tunapopataka au kwanini inarudi nyuma, lakini kumbe makocha kwenye hizi klabu ndio wanaotakiwa kunoa makali yao ya ufundishaji ili kuwaongezea ubora wachezaji nao wakatusaidie kwenye timu yetu pendwa ya Taifa.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s